Acts 9:19-22

19 aBaada ya kula chakula, akapata nguvu tena. Sauli akakaa siku kadhaa pamoja na wanafunzi huko Dameski.

Sauli Ahubiri Dameski

20 bPapo hapo akaanza kuhubiri kwenye masinagogi kwamba “Isa Al-Masihi ni Mwana wa Mungu” 21 cWatu wote waliomsikia Sauli walishangaa na kuuliza, “Huyu si yule mtu aliyesababisha maangamizi makuu huko Yerusalemu miongoni mwa watu waliolitaja jina hili? Naye si amekuja hapa kwa kusudi la kuwakamata na kuwapeleka wakiwa wafungwa mbele ya viongozi wa makuhani?” 22 dSauli akazidi kuwa hodari na kuwashangaza Wayahudi walioishi Dameski kwa kuthibitisha kuwa Isa ndiye Al-Masihi.
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.

Copyright information for SwhKC